Nabii na Mchungaji milionea nchini Malawi, Shepherd Bushiri na mke wake Mary wamejisalimisha kwa polisi mapema leo jumatano Novemba 18, katika mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, baada ya kukwepa masharti ya dhamana nchini Afrika Kusini.

Awali mwezi huu, wanandoa hao waliachiwa kwa dhamana na mahakama moja nchini Afrika Kusini baada ya kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi na utakatishaji wa pesa.

Mchungaji huyo ambaye awali, alisema kuwa alitaka kutakasa jina lake, kupitia mitandao ya kijamii siku ya Jumamosi aliwaambia wafuasi wake kuwa, uamuzi wake wa kukiuka dhamana ni kwasababu alipokea vitisho vya kifo.

Muhubiri huyo pia alishtumu Afrika Kusini, kwa kushindwa kuwapa ulinzi.

Siku ya Jumatatu Afrika Kusini ilitoa kibali cha kukamatwa kwa Bushiri ambaye alitoroka nchini Afrika Kusini, katika hali ya utata ingawa tetesi zinadai alitoroshwa katika msafara wa Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera.

Viongozi wa Al-Shabaab wapigwa marufuku kuingia Marekani
Kaseja na wenzake warejea KMC FC