Tito Onesmo Machibya anayejulikana kama ‘Nabii’ Tito (44) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong’ona Manispaa ya Dodoma amepandishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya kwa shtaka la kutaka kujiua

Amepandishwa kizimbani kwa kosa kutaka kujiua mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo alijichana chana na wembe katika baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati Jeshi la Polisi likifanya uchunguzi nyumbani kwake.

Aidha, Nabii Titoo alikamatwa Januari 23, 2018 na jeshi la polisi akituhumiwa kufanya uchochezi na baadaye alipelekwa kupimwa akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili (Mirembe) na kufahamika kuwa mtu huyo alikuwa na matatizo ya akili.

Hata hivyo, Jeshi la polisi liliendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake na siku jeshi hilo lilipokwenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake ndipo alifanya jaribio la kutaka kujiua.

 

Rais Magufuli akutana na Dkt. Slaa Ikulu, wateta
Moto wateketeza basi