Meneja wa klabu ya West Ham, Slaven Bilic ameweka mkakati wa kukiboresha kikosi chake kwa kutenga kiasi cha Pauni milioni 20, kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Olympic Lyon, Nabil Fekir.

Bilic anaamini usajili wa mchezaji huyo endapo utafanikiwa, kutakua na muamko tofautio katika mfumo ambao anatarajia kuutumia msimu ujao wa ligi ambapo kikosi cha The Hammers, kitakua kikicheza katika uwanja mpya wa Olympic uliopo jijini London.

Bilic amekua akimfuatiliwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, na amejiridhisha anaweza kushirikiana na Dimitri Payet ambaye msimu uliopita alionyesha uwezo wa kustaajabisha kwa kuifungia mabao muhimu West Ham Utd.

Video: Walichozungumza CCM Baada ya Upinzani Kuilalamikia Serikali Kwa Wananchi
Hesabu Za Antonio Conte Zashabihiana Na Kwadwo Asamoah