Kiungo wa majogoo wa jiji Liverpool, Naby Keita amesema anaendelea vizuri baada ya kufikishwa hospitalini usiku wa kuamkia leo, kufuatia majeraha ya mgongo alioyapata akiwa katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya SSC Napoli.

Mchezo huo uliomalizika kwa Liverpool kufungwa bao moja kwa sifuri, ulishuhudia kiungo huyo kutoka nchini Guinea, akipata majeraha hayo dakika ya 19 na baadaye kukimbizwa hospitali ya mjini Naples kwa matibabu zaidi.

Mapema hii leo Kaita alithibitisha kuendelea vizuri, na anaamini matibabu aliyopatiwa tangu alipofika katika hispitali ya mjini Naples-Italia, yamemsaidia kurejea katika hali yake ya kawaida, japo atahitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa madaktari wa klabu ya Liverpool.

Kabla ya mchezaji huyo kuthibitisha anaendelea vyema, daktari mkuu wa klabu ya Liverpool alionyesha kuwa na wasiwasi na hali ya Keita, huku akiwataka waandishi wa habari kuwa na subra.

“Keita anapatiwa matibabu, tutawapa taarifa zaidi baadae, kwa sasa hatuwezi kusema lolote kwa sababu hakuna anaejua nini kilichomsibu, zaidi ya kusubiri majibu ya vipimo alivyofanyiwa.” Alisema daktari, mara baada ya mchezo dhidi ya SSC Napoli.

Liverpool have confirmed Naby Keita is 'fine' after going off in NaplesNaby Keita akiugulia maumivu ya mgongo.

Leo mchana Keita alitarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitali na kuanza safari ya kurejea jijini Liverpool-England.

Hata hivyo mpaka sasa hakuna taarifa zinazoeleza kama kiungo huyo ataweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Man City katika mchezo wa ligi kuu ya soka cnhini England, mwishoni mwa juma hili.

Keita, alisajiliwa na Liverpool akitokea RB Leipzig kwa ada ya Pauni milioni 48, mwishoni mwa msimu uliopita, na mpaka sasa ameshacheza michezo tisa ya ligi ya England, huku akianzishwa kwenye kikosi cha kwanza mara nne.

Eliud Ambokile aibuka kidedea mwezi Septemba
Afariki kwa kuongeza makalio