Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (Nacte) limesema litavifutia baadhi ya vyuo vikuu nchini baada ya kufanya tathmini ya kuangalia ubora wa vyuo hivyo na kuongeza kuwa  tahthmini hiyo imefanywa na jopo la wataalam waliobobea katika nyanja mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila alipokuwa akizungumza waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Msanjila amesema tathmini imefanyika  kwa lengo la kuboresha mfumo wa elimu nchini na kuongeza kuwa tathmini hiyo imefanyika ili kuweza kubaini vyuo vyenye sifa na visivyo na sifa na baadhi ya vyuo vitafungiwa.

“Lengo la Serikali ni kuwa na vyuo vinavyotoa  elimu bora  kwa wanachi wake, mwaka huu tupo makini na hatuta pepesa macho pembeni kwa vyuo ambavyo havina sifa”alisema Prof. Msanjila.

Hata hivyo Prof .Msanjila amesema kuwa vyuo vitavyofutiwa usajili  wanafunzi wake watahamishiwa katika vyuo vingine vyenye sifa na wale wataokao kosa sifa hawataweza kuendelea na masomo.

Prof. Ndalichako: Maadili ni jukumu la jamii nzima
Viongozi wa dini wamtaka Makonda kumuomba radhi Kamanda Sirro