Rafael Nadal amefanikiwa kushinda taji la US Open kwa kumchapa mpinzani wake kutoka nchini Urusi, Daniil Medvedev katika fainali iliyokua ya ‘vuta nikuvute’.

Nadal ameshinda taji la US Open kwa mara ya nne, akifanya hivyo mwaka 2010, 2013 na 2017, na sasa anafikisha mataji 19 ya Grand Slam.

Mcheza Tennis huyo kutoka nchini Hispania mwenye umri wa miaka 33, alimshinda Medvedev kwa seti tatu kwa mbili, ambazo ni 7-5, 6-3, 5-7, 4-6 na 6-4.

Hata hivyo, haikua kazi rahisi kwa Nadal kupata mafanikio hayo, kwani ilimlazimu kusubiri kwa muda wa saa nne na dakika 50 kumuangamiza mpinzani wake, ambaye alionekana kuwa makini kwa kuonyesha upinzani wa kweli.

Wakati huo huo, mwanadada kutoka nchini Merekani Serena Williams, mwishoni mwa juma alishindwa kufurukuta mbele ya Bianca Andreescu, katika mchezo wa fainali wa michuano ya US Open.

Serena anaeshika nafasi ya tisa kwa ubora duniani upande wa wanawake, alikua akipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, lakini kilichotokea mashabiki wengi duniani hawakuamini.

Image result for Bianca AndreescuBianca Andreescu

Serena alipoteza mchezo huo kwa kufungwa seti mbili kwa sifuri, ambazo ni 6-5 na 7-5, dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini Canada, ambaye anapanda kwa kasi kubwa katika viwango vya ubora wa mchezo wa Tennis duniani.

Mara baada ya kutwaa taji la US Open kwa mara ya kwanza katika maisha yake hapo jana, Andreescu mwenye umri wa 19, alisema ni ndoto ambayo alikuwa akiiota kwa muda mrefu, na hana budi kumshukuru mungu, kwa kufanikisha ndoto hiyo.

“Siamini kama ndoto yangu imetimi, kumshinda mchezaji kama Serena si jambo dogo, najivua kufikia hatua hii katika maisha yangu, nimefurahi sana,” alisema Andreescu.

Kinda huyo amevunja rekodi ya Maria Sharapova, ambaye aliwahi kutwaa taji la US Open, akiwa na umri wa miaka 19 mwaka 2006.

Kwa sasa Andreescu anashika nafasi ya 1035 kwa ubora duniani, na kwa mafanikio aliyoyapata, anatarajiwa kupanda maradufu katika viwango vya ubora wa mchezo huo, upande wa wanawake.

Serikali yataja waliopoteza maisha kwa ajali za ‘bodaboda’, ni hatari
Queen Latiffa ataka Nicki Minaj aachwe apumzike