Mcheza tenisi namba moja duniani Rafael Nadal amelazimika kujiondoa kwenye michuano ya Paris Masters baada ya kuumia goti.

Mhispania huyo alitakiwa kushuka dimbani leo kucheza na Serb Filip Krajinovic katika mchezo wa robo fainali, lakini tatizo la goti limemweka nje ya michuano hiyo inayoendelea barani Ulaya

Aidha, Nadal alipata maumivu hayo ya goti raundi ya tatu kwenye ushindi wake dhidi ya Pablo Cuevas. Ushindi huo ulimpa nafasi ya kucheza robo fainali lakini sasa hatocheza kutokana na maumivu hayo.

Hata hivyo Nadal amesema kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anarejea kwenye fainali za dunia za ATP jijini London, ambazo zinaanza Novemba12-19 mwaka huu ili kuweza kujiweka vizuri katika nafasi yake.

Mmarekani afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujaribu kuipindua serikali
Chadema: Tunauhakika tutashinda jimboni kwa Nyalandu