Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed amewataka Wananchi wa Mtwara na mikoa ya karibu kujitokeza kwa wingi Aprili Mosi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ili kuungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mkufunzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Mswadiku (kulia) akifafanua jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Mwita (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed wakati wakikagua maandalizi katika uwanja huo.

Akiwa katika ukaguzi huo, Waziri Ndalichako aliambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Mwita, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu.

Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt, Islam Seif, Katibu Mkuu wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Rajab pamoja na viongozi mbalimbali katika mkoa huo.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa.”

Serikali kuja na mradi wa Bilioni 119: Waziri Mkuu
Waziri Mkuu azindua jengo Wagonjwa wa dharula