Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami ameelezea kusikitishwa kwake na maneno aliyoyatoa mtangazaji maarufu wa redio nchini humo Jalang’o, akiyazungumzia mahusiano ya kimapenzi ya msanii huyo hadi kujikuta akitoa siri za ndani.

Kinyume na matakwa ya Nadia, wakati wa kipindi chake cha asubuhi ambapo alidai kuwa msanii huyo alikuwa akificha ujauzito wake na mwanamuziki Arrow boy.

Baada ya kusambaa kwa kasi kwa taarifa hizo, Nadia aliutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuchapisha video akisimulia alivyoumizwa na kitendo cha Jalango kuvujisha taarifa zake zisizopaswa kuwekwa hadharani.

Akimzungumzia Jalang’o, Nadia alisema kuwa alichokifanya mtangazaji huyo ni kitendo cha ajabu na cha hadhi ya chini zaidi ambacho hakupaswa kufanya mtu wa aina yake.

Msanii huyo aliangazia zaidi matamshi ya Jalang’o wakati wa kipindi chake, akiweka wazi kuwa aliwaalika nyumbani kwake msanii Nadia Mukami pamoja na Arrow Bwoy ili tu awafahamu kwa undani hasa kuhusu mambo yao waliyoamua kuyaweka faragha.

Nadia amesema alisita kuitikia wito wa mtangazaji huyo lakini baadaye akakubali kwenda baada ya Arrow Bwoy kumsisitiza waende pamoja.

“Ulichofanya ni makosa kabisa, kusema ukweli. Nisingejali, hata kama wewe  ni mtu wa blogu, mtangazaji au shabiki. Lakini ulitualika nyumbani kwako, ili ufungue mdomo wako na kinachofuata ni kuhalalisha makosa uliyoyafanya na kusema haujutii,” alisema Nadia.

Nadia Mukami aliendelea kweka wazi kwamba yeye na Arrow Bwoy wamepitia mambo mengi katika maisha yao na ikafika pahala wakachagua kuweka mambo yao mengi yenye kuwahusu kuwa ya siri.

Hivyo kitendo cha Jalango kuvujisha taarifa za ujauzito wa Nadia na Arrow boy kimetafsiriwa kama kuwakosea heshima kwa kujivika mamlaka ya kuwa msemaji wa familia yao jambo walilolipinga vikali.

Milioni 346 kwa atayempata Muuaji wa Young Dolph
Wabunge waitwa Dodoma