Nahodha wa Mabingwa wa Soka nchini Guinea Horoya AC Ocansey Mandela amesema jambo lililowaleta Tanzania ni moja tu, kushinda mchezo dhidi Simba SC, ili wajisafishie njia ya kutinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, msimu huu 2022/23.

Horoya AC itakua mgeni wa Simba SC leo Jumamosi (Machi 18) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ukiwa mchezo muhimu kwa pande zote mbili, ambazo zinahitaji ushindi.

Mandela amesema anaamini maandalizi yao kuelekea mchezo wa leo yanatosha kuishangaza Simba SC, kama ilivyowahi kushangazwa katika baadhi michezo ya Kimataifa kwenye wao wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Hatuwezi kutoka Guinea kuja kupoteza, tumekuja kushinda ili tujisafishie njia ya kwenda Robo Fainali, na kama ambavyo timu zingine zimepata matokeo hapa basi hata sisi tutapata matokeo pia mashabiki wao wajiandae kisaikolojolia”

“Tupo kwenye Michuano hii kwa ajili ya kupambana, tumejiandaa vizuri kuikabili Simba SC ambayo tunaiheshimu sana kwa sababu ipo nyumbani kwao, tunajiamini kwa kuwa tumejiandaa kushinda hapa Dar es salaam.” Amesema Mandela

Endapo Simba SC itashinda leo Jumamosi (Machi 18) dhidi ya Horoya AC itafikisha alama 09 na kutinga moja kwa moja Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na kuungana na Raja Casablanca ya Morocco iliyojikusanyia alama 12 hadi sasa.

Na ikitokea Horoya AC inaibuka na ushindi dhidi ya Simba SC, Miamba hiyo ya Guinea itafikisha alama 07, ambazo zitaifanya kusubiri hadi katika mchezo wa mwisho wa Kundi C utakawakutanisha dhidi ya Vipers SC ya Uganda nyumbani kwao, ili kujua hatma yao.

Utunzaji Mazingira: Jafo awapa dozi Wakuu wa Wilaya
Wachezaji Simba SC waahidiwa Milioni 250