Nahodha wa kikosi cha Polisi Tanzania FC Tariq Simba amesema wamepambana kwa uwezo wao lakini haikuwa riziki wanakubali wanajipanga kwa Ligi ya Championship.

Hadi inashuka Ligi Kuu, Polisi Tanzania imecheza michezo 29 na kushinda sita, sare saba na kupoteza 16 ikishika nafasi ya 15 na pointi 25, huku leo ikitarajiwa kumalizana na Azam jijini Dar.

Nahodha huyo alisema walijaribu kuipambania timu kuhakikisha inashinda katika michezo yake lakini imekuwa bahati mbaya baadhi walipoteza.

“Tumepambana kwa kila hali tumevuja jasho letu kuhakikisha tunapata matokeo lakini imekuwa ngumu, tunajipanga,” alisema kiungo huyo ambaye amewahi kuzichea timu za Tunduru Korosho na Biashara United.

Kocha wa Polisi, Mwinyi Zahera amesema yapo mambo mengi yamechangia timu hiyo kufika hapo.

Zahera alikabidhiwa kikosi hicho Desemba 2 mwaka jana baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga ya ukurugenzi wa maendeleo ya soka la vijana na wanawake akichukua nafasi ya Joslin Bipfubuza aliyetimuliwa Oktoba 27 kutokana na matokeo mabovu ya klabu hiyo.

Tanzania, Burundi zakubaliana ulinzi rasilimali Ziwa Tanganyika
Kiswaga awapongeza wajumbe Kamati za kudumu za Bunge