Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha), Gertrude Ndibalema amejiuzulu wadhifa huo kuanzia jana Machi 11,2018.

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 ametangaza kujiuzulu kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi.

“Kwa kuwa nakipenda chama changu na kwa taaluma yangu ya mawasiliano kwa umma, ili kuepuka mgongano, nimeamua kukaa pembeni ili kutimiza azma yangu na nitabaki kuwa mwanachama,” amesema Ndibalema.

Hata hivyo, Gertrude ni kiongozi wa pili wa ngazi ya juu Bavicha kujizulu akitanguliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi aliyejiunga na CCM.

Mama ajinyonga baada ya kuua wanawe wanne
Hongera Chege kwa kupata kabinti