Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson ameungana na wanawake wa Kanisa la Tanzania Assembles of God TAG Makambako na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni saba zitakazo saidia ujenzi wa kanisa hilo.

Akiwa katika ibada ya maadhimisho ya sikukuu ya wanawake watumishi wa Kristo wa kanisa hilo lililopo mjini Makambako,Dkt. Tulia kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge mkoani Njombe na wanawake wa kanisa hilo amesema kuwa wameshirikiana kukusanya fedha hiyo ili kuonyesha ushiriki wao katika Baraka ya ujenzi wa kanisa.

“Katika kitabu cha methali 31 kinazungumzia mama kufanya yampasayo kufanya, lakini kama wanawake tumepewa kazi ya kuwalinda wanaume na kwa maana hiyo tupaswa kuilinda jamii yetu, taifa letu na ulimwengu mzima unatutegemea sisi hasa wanawake wakristo wamchao bwana,”Amesema Dkt. Tulia

Kwa upande wake makamu Askofu wa T.A.G Njombe kaskazini ambaye pia ni mchungaji wa kanisa hilo, Patrick Luhwago amesema kuwa ili mwanamke aweze kufanikiwa katika utumishishi uliotukuka ana wajibu wa kujifunza kwa watu waliotangulia na waliofanya vizuri.

Naye mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwa kuiwezesha halmashauri ya mji huo kupata fedha za miradi mbali mbali ukiwemo mradi wa ujenzi wa hospital.

Video: Msiba wa Ruge wageuka kuwa fursa, Mvua nzito ya mawe yanukia
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 4, 2019