Serikali imetangaza kuyatoza faini makampuni ya simu nchini kutokana na kukiuka sheria na utaratibu wa ajira kwa raia wa kigeni kwa kuwaajiri kufanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na raia wa Tanzania.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde alibaini kuwepo kwa wafanyakazi wa kigeni katika makampuni hayo walioajiriwa kufanya kazi za kufunga meza na viti, kazi ambazo hata watanzania wangeweza kuzifanya.

Anthony Mavunde akila kiapo mbele ya rais John Magufuli

Anthony Mavunde akila kiapo mbele ya rais John Magufuli

“Lakini pia kuna wageni ambao wako katika hii kampuni yenu, wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania, kwa mfano huyu anayefunga viti, hii kazi inafanywa na vijana wetu…kibali chake kinaisha kesho, naagiza asipewe kingine na aondoke,” Mavunde anakaririwa.

Katika ziara yake iliyolenga kufanya ukaguzi wa vibali vya ajira kwa wageni, Mavunde alibaini pia uwepo wa raia wa Vietnam wanaofanya kazi katika kampuni ya simu ya Halotel bila kuwa na vibali vya kuishi nchini wala vibali vya kufanya kazi. Pia, alibaini uwepo wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao hawajapewa mkataba wa ajira huku waliopewa mikataba ya ajira hawakupewa nakala ya mikataba yao kinyume cha sheria.

Baada ya kubaini uwepo wa mapungufu hayo, Mavunde aliagiza uongozi wa Halotel kuhakikisha wanawapa mikataba wafanyakazi wao wote na kuzipeleka nakala za mikataba hiyo ofisini kwake.

 

 

Rais Wa TFF Afunga Mwaka 2015 Kwa Zawadi
Steven Naismith Kuondoka Goodson Park