Mkurugenzi wa maji safi na usafi wa mazingira mjini Igunga Raphael Merumba amesimamishwa kazi na Naibu waziri wa Maji Juma Aweso baada ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kulalamikia kuwa anawafanyia unyayasaji ikiwemo kuwadai rushwa ya ngono.

Naibu waziri Aweso amefikia maamuzi hayo ya kumsimamisha kazi mkurugenzi na bodi yake nzima kupisha uchunguzi akiwa katika ziara mkoani humo.

Ambapo alifanya kikao cha ndani na wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo na ndipo walipoanza kumueleza changamoto wanazokutananazo ikiwemo mkurugenz huyo kuwaomba wafanyakazi wake rushwa ya ngono.

“Kwahiyo hapa tumepata maelezo ya Wafanyakazi lakini kwa kipindi hiki Mkurugrenzi, Mwenyekiti na Bodi yako mtupishe kidogo, wakurugenzi wa Mamlaka za Maji msinyanyase wafanyakazi wenu, na kwa yoyote atakayenyanyasa wafanyakazi wake sisi hatutamchekea”, amesema Naibu Waziri Aweso.

Leo tena donge nono- Waziri Mpango
Lusajo 'huyooo...' KMC FC