Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amenusurika baada ya gari alilokuwa amepanga kuanguka jana katika eneo la Iguguno, mkoani Dodoma.

Katika gari hilo, kulikuwa na abiria wengine saba, akiwemo mtoto mdogo lakini taarifa zimeeleza kuwa hakuna ambaye alipata madhara makubwa licha ya gari hilo kupinduka mara nne.

Naibu waziri Nditiye ameielezea ajali hiyo kuwa ilikuwa mbaya lakini anashukuru Mungu kuwa watu wote walinusurika.

“Kwenye gari kulikuwa na watu saba na mtoto mmoja. Nashukuru Mungu hakuna madhara ya mtu kuumia. Wote tuko salama licha ya kuwa gari lilibinuka zaidi ya mara nne,” Nditiye anakaririwa na Mwananchi.

Gari hilo ambalo limeonekana kuharibika vibaya, limeonekana katika picha likiwa halina tairi moja la mbele la upande wa kulia. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijaelezwa.

Waitara aanza uteule wa unaibu waziri kwa ‘onyo kali’
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 12, 2018