Naibu Waziri – TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo akiongozana na Naibu Katibu Mkuu – TAMISEMI Dr. B.M. Makali wamefika Mkoani Lindi kuembelea Shule ya Sekondari Lindi iliyopata janga la moto.

Mh. Naibu Waziri alifika shule ya sekondari Lindi naa kujionea majengo ambayo yameungua na moto ambapo pia alielezwa jitihada mbalimbali ambazo zimechukuliwa na Serikali ya Mkoa.

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa wanafunzi wote wahakikishe wanaripoti shule kwa wakati kwani serikali ya Mkoa imeshajipanga katika kukabiliana na changamoto iliyopo ya madarasa yaliyoungua. Pia amewataka wazazi na walezi wote kutokuwa na hofu kwani majengo mengine ya shule yapo salama.

Vilevile amewaomba wananchi na wadau mbalimbali kwa ujumla kuchangia fedha na mali zitakazosaidia katika kukarabati miundombinu ya shule. Pia, alieleza kuwa serikali imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule za sekondari 33 za zamani.

 

Video: Waziri Mahiga amepokea msaada wa maadawati
Video: Mpango wa Usambazaji Umeme Tanzania Nzima Wazinduliwa