Naibu waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amewataka wadau wa sekta ya Habari na Mawasiliano nchini kutumia fursa ya uwepo wa maafisa uhusiano na wadau wa sekta hiyo kutoka mataifa mbalimbali, kuimarisha mfumo wa utoaji habari na mawasiliano katika maeneo yao ya kazi.

Mhandisi Kundo ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua mkutano mkuu wa maafisa uhusiano na mawasiliano kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, mkutano utakaofanyika hadi tarehe 27 mwezi huu.

Amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini, ni fursa kwa watanzania na utazidi kufungua milango zaidi kwa wawekezaji kwenye sekta ya habari na mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa habari kutoka kwa maafisa uhusiano na mawasiliano nchini.

Mkutano huo mkuu wa 33 wa maafisa uhusiano na mawasiliano Afrika umelenga kujadili changamoto mbalimbali katika sekta hiyo na una washiriki kutoka zaidi ya mataifa ishirini barani Afrika.

Watatu wafariki dunia katika ajali ya basi Manyara
Miaka 3 jela kwa kuwanyanyasa kingono yatima kwenye kituo chake