Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amewakabidhi vifaa vya kujilinda na ngozi watu wenye ulemavu wa ngozi katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Ametoa vifaa hivyo baada ya kuombwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi katika wilaya za mkoa wa Kagera.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa hivyo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameipongeza wilaya ya Karagwe kwa kuona uhitaji wa kuwapatia vifaa vya kujilinda.

Amesema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana changamoto nyingi lakini wilaya ya Karagwe imeona umuhimu wa kuwapatia walemavu hao vifaa vya kujikinga jua na ngozi na kueleza kuwa hilo ni jambo jema linaloweza kuwapa faraja watu wenye ulemavu.

Aidha, amesema kuwa uamuzi wa kuwapatia vifaa ni jambo jema na tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli alishaliona hilo na katika Baraza lake la kwanza la Mawaziri alimteua mtu mwenye ulemavu wa ngozi kushika nafasi ya uwaziri.

Kwa mujibu wa Dkt. Mabula, kuwa na ulemavu wa ngozi hakumfanyi mtu mwenye ulemavu huo kushindwa kufanya kazi na kusisitiza kuwa cha msingi ni kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Godfrey Mheluka amesema kuwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi kutembelea wilaya yake kwa ajili ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi ameona atumie fursa hiyo kuwapatia walemavu wa ngozi vifaa lengo ni kuonesha kuwajali watu hao

Nassari ajibu kuhusu kuvuliwa Ubunge
Video: Spika afunguka kufyeka mshahara na posho za Lissu, JPM amwokoa aliyebambikiwa kesi ya mauaji

Comments

comments