Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Masauni anakuwa mwanachama wa 16 wa chama hicho kujitosa kwenye kinyang’anyiro.

Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu hiyo, Masauni amesema kuwa nafasi ambayo aliaminiwa na wananchi, nafasi ambayo aliteuliwa na Rais na nafasi nyingine za uongozi katika serikali na chama chake zimemjenga vya kutosha na yupo tayari kuwa Rais wa Zanznibar.

Amesema kuwa endapo chama chake kikampitisha kuwa mgombea, na wananchi wakamchagua kuwa Rais wa Zanznibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, atahakikisha anakidhi matakwa yao kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya Taiafa.

Aidha ameahidi kutumia mbinu za kisasa kuhakikisha anatekeleza mkakati wa kupunguza umasikini kwa Wazanzibar wote.

JPM apiga marufuku ujenzi wa stendi Arusha karibu na CCM "ya watanzania wote"
RPC na Mkuu wa TAKUKURU waponea tundu la sindano fagio la Magufuli Arusha