Naibu waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Ametoa wito kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.

Mpina aliyasema hayo, alipotembelea taasisi ya Muungano ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa  Zanzibar, iliyopo chini  ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada  ya Kukagua jengo jipya la taasisi hilo ambalo halijaanza kutumika ikidaiwa ni kutokana na changamoto mbalimbali pamoja na ukosefu wa samani, Naibu Waziri Mpina aliishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo ya kusaidia watanzia wanaoishi katika ukanda wa pwani ili kuwawezesha kusaidia kuinua uchumi wao na kuongeza pato la taifa.

Aidha, Mpina aliongeza kuwa anategemea tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zitoe muongozo kwa serikali na ambavyo nchi inavyoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. “Hakikisheni serikali inapata taarifa zenu ili ziweke kutumika, mpo kimya sana na hamsikiki.” Alisisitiza Mpina.

Kwa upande mwingine taasisi hiyo imekuwa pia ikitoa nafasi kwa wanafunzi wageni toka katika nchi mbali mbali duniani kuja kujifunza na kufanya tafiti juu ya viumbe hai waishio baharini  aina ya  Pomboo (Dolphin)ili kuweza kufahamu mazingira na tabia za ndani za viumbe hao na kubadilishana uwezo na kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupitia malipo ya mafunzo hayo maalum. Naibu Waziri Mpina pia, alitoa Pongezi kwa taasisi hiyo kuwa na jengo zuri pamoja na changamoto wanazokabilana nazo na kuwashauri wahamie na kuanza kulitumia jengo hilo. Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar pamoja na kumuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, inahusisha pia kutembelea baadhi ya taasisi za muungano mjini humo.

Shkodran Mustafi Aondolewa Kikosini
Uongozi Wa Simba Watoa Shukurani, Waipiga Kijembe Yanga