Kiwanda cha kutengeneza vyuma cha MMI Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa kulipa faini hiyo baada ya siku saba kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kwa kutiririsha maji machafu katika maeneo ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa. Maji ambayo ni hatari kwa mazingira na viumbe hai.

Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea eneo la  mtaa wa viwanda mikocheni kufuatia uchafuzi wa mazingira unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka katika maeneo hayo.

Wakati huohuo, Shirika la maji safi na majita taka Jijini Dar es Salaam na Pwani  ( Dawasco) limepewa siku kumi na saba kumaliza tatizo la utiririshaji wa maji taka katika mtaa wa TPDC mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam.

Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi wa tatu na kutoa siku saba kwa DAWASCO na NEMC kusimamia suala zima la usafi wa mazingira na agizo lake kuupuzwa.

Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi wa mazingira hauwezi kuendelea kuvumiliwa na lazima hatua za kisheria zichukuliwe, na kuwaasa watendaji wa taasisi za serikali kuyapa kipaumbele maagizo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu za serikali kinyume na hapo ni kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali lazima zifanye kazi kwa kushirikiana kutokana na kwamba kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco na Manispaa ya kinondoni katika suala zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira katika mtaa wa TPDC.” Alisema.

Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa  ifikapo tarehe 30/7/2016  asikutane tena na tatizo la uchafu na harufu mbaya katika mtaa wa TPDC kwani hali hiyo ni hatari sana kwa afya ya wakazi wa maeneo hayo na mazingira.

Kwa upande wake DAWASCO ikiwakilishwa na Injinia Erick Jackson alisema kuwa Tangu muheshimiwa Naibu Waziri Mpina atoe agizo la uondoshwaji wa majitaka na uboreshwaji wa miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa wakifanya kazi na bado inaendelea na kazi hiyo  pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha na ufundi.

Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kinondoni umelishitaki shirika la maji safi na maji taka jijini dar es salaam na Pwani DAWASCO ,kiwanda cha MMI steel na Tembo Tiles kwa uchafusi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka

Tanzia: Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki auawa
Wimbo Mpya: Roma ft Jos Mtambo & Darassa - Kaa Tayari