Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga Jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori.

Dkt. Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Amesema, Serikali imeliona tatizo hilo na itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga.

“Nimekuja kuwapa pole, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa hivyo nawaomba muendelee kuwa wavumilivu kipindi hiki ambacho Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto na wanaomba mpokee salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa anawapenda sana,” amesema Dkt. Mollel.

Mmoja wa madereva Japhet Jeremiah amesema, wamekuwa wakiombwa kiasi cha shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, jambo ambalo ni wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania ambao hadi wanafikia hatua ya kugoma.

Kahata: Moto wa Simba SC utakuwa zaidi ya ule wa mara ya kwanza
Maamuzi ya TFF yaikuna Mtibwa Sugar