Mfanyabiashara raia wa Marekani, Jason Spindler ambaye anatajwa kuwa alinusurika katika shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2011, ni mmoja kati ya watu 14 waliouawa jana na magaidi kwenye jengo lenye hoteli ya Dusit 2, 14 Riverside jijini Nairobi nchini Kenya.

Spindler ambaye alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya I-Dev International, alinusurika katika shambulizi lililofanywa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda likiongozwa na Osama Bin Laden, baada ya ndege zilizotekwa kugongeshwa kwa makusudi kwenye majengo mawili jijini Washington DC na New York ambapo watu 3,000 walipoteza maisha.

Mama yake Spindler ameliambia Shirika la Habari la NBC kuwa wamesikitika kumpoteza kijana wao ambaye alikuwa na umri mdogo.

Taarifa ya kitengo cha Ubalozi wa Marekani nchini Kenya kimethibitisha kuwa raia wa Marekani ni mmoja kati ya watu waliouawa kwenye shambulizi hilo la Nairobi lakini haitoa taarifa zaidi.

“Tunamkumbuka sana. Na tunasikitishwa sana kuona maisha ya kijana huyu mdogo mwenye maarifa mengi yakikatishwa na ugaidi. Alikuwa akijaribu kuleta mabadiliko chanya kwenye dunia ya tatu kupitia masoko yaliyopo,” amesema mama yake, Sarah Spindler.

Ndugu zake wameweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii na kueleza namna ambavyo watamkumbuka mhanga huyu wa tukio la kigaidi la Septemba 11, 2011.

Katika shambulizi hilo la jana, watu 14 wameripotiwa kupoteza maisha na makumi wamejeruhiwa. Vikosi vya usalama vya Kenya vilifanikiwa kuwadhibiti na kuwaua magaidi wote waliovamia jengo hilo, kwa mujibu wa Rais Uhuru Kenyatta.

Kundi la kigaidi la Al Shabaab lilikiri kuhusika na tukio hilo.

Video: Mapya ya ugaidi Kenya, Kuna giza nene uchaguzi ujao
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 17, 2019