Mpenzi wa Barakah Da Prince, Naj amemchoma mwanafamilia wa WCB, Romy Jones baada ya kumtumia jumbe za kumshawishi wachepuke.

Mawasiliano ya wawili hao yaliwekwa wazi dakika chache baada ya Barakah kugeuka mbogo kwenye Instagram jana akiweka picha ya Romy na kuandika, “Daaah unaonekana mwana kumbe pimbi tu….Na hata hilo vazi ulilovaa unalitia aibu shenzi typ soon nakutia aibu jamaa… next post nakutia aibu wack wewe…”

Hata hivyo, kabla Barakah hajaanika ‘cha kuanika’ kuhusu Romy, dada yake Naj aitwaye Lady Naa alipoweka wazi mawasiliano ya jumbe za ndani kupitia Instagram (DM)kati ya Naj ambaye hivi sasa yuko Uingereza na Romy.

Kwa mujibu wa ‘screenshot’ za mawasiliano hayo, Romy ndiye aliyeanza kumuamsha Naj akimueleza kuwa ana mpango wa kwenda Uingereza hivi karibuni. Alimtaka Naj kama ikiwezekana waandae matamasha kadhaa huko.

Lakini mazungumzo ya biashara yaliyoanzishwa yaligeuka baada ya Romy kumuulizia Barakah Da Prince kwa uchokozi na kisha kuwasilisha ombi lake la kumfanya Naj kuwa mchepuko kwani Romy tayari ni mwana ndoa.

“Hivi Barakah yupo kwanza?” aliuliza Romy. “Yes I’m still with my prince,” Naj alijibu.

“Mmmhh…. Eti my prince, anakupa nini prince wako, U can be my side chick and I will take good care of u na pia utajulikana vilevile, what do you think.”

LOL… That’s sooo stupid Rommy. Naachaje roho yangu kwenda kuwa a lame a*s side chick,” Naj alikataa kwa hasira na kejeli ofa ya Romy.

Hata hivyo, Romy ambaye alipotezea swali kuhusu mkewe, huenda alimkera zaidi Barakah aliyetumiwa jumbe hizo baada ya kumchana kuwa anashusha nyota ya mrembo huyo.

“Ila kiukweli BARAKAH anashusha nyota yako, Trust me,” aliandika Romy.

Wiki hii Naj anaungana na Harmonize kuweka wazi jumbe zilizokuwa zimetumwa kwao kwa wakati tofauti na watu waliokuwa wanalenga kuvuta mioyo yao kutoka kwa wapenzi wao.

Harmonize alimpa nafasi Sarah kuziona jumbe alizotumiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Jackline Wolper akikumbushia nyakati za shangwe za mapenzi yao. Sarah aligeuka mbogo kama ilivyokuwa kwa Barakah.

Video: Ripoti ya CAG yawaweka kona mawaziri watano, Waziri Ummy ataka faragha kwa Makonda
Trump aitaka Urusi kujiandaa na mashambulizi

Comments

comments