Wanawake wenye umri wa miaka 21 au zaidi wanashauriwa kufanya kipimo cha saratani ya mlango wa kizazi ( cervical cancer screening) kila baada miaka mitatu.

Hospitali mbalimbali nchini zikiwemo Ocean Road, Muhimbili, Mbeya, KCMC, Bugando, Agha Khan zina vifaa maalumu kwa ajili ya kutoa huduma ya vipimo vya ugonjwa  huu.

Ugonjwa wa saratani huanza pale seli za mwili zinapokuwa bila mpangilio na kusababisha uvimbe ambao huweza kusambaa sehemu mbalimbali za mwili.

Ugonjwa huu wa saratani huanza taratibu bila maumivu yeyote na huchukua muda kabla ya kuonyesha dalili.

Vitu vinavyochangia ukuaji wa saratani ni pamoja na virusi, bakteria, parasiti, madini mazito mfano asbestos pamoja na mionzi.

Saratani huambatana na dalili zifuatazo, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito bila sabau na uchovu bila kufanya kazi, uvimbe wa zaidi ya wiki tatu maeneo kama, shingoni, kwapani, tumboni, kwenye matiti.

Matiti kubadilika umbile, ngozi kukunjama, au chuchu kutoa majimaji au damu, Mabadiliko katika kupata haja kubwa, kutokwa na damu haja kubwa na ndogo, puani au kwenye makohozi, kwenda haja ndogo mara kwa mara, isivyo kawaida, au choo kidogo kutoka kwa shida.

Mwanamke kutokwa na ute, maji maji, usaha, damu, wakati wa kujamiana, baada ya kukoma hedhi au nje ya mzunguko wa hedhi, maumivu wakati wa kula au kunywa, kukohoa au kuwa na sauti ya kukwaruza kwa zaidi ya wiki tatu.

Kuna namna tofauti ya kujikinga na saratani, ikiwa pamoja na epuka kuwa na uzito uliokithiri kwa kufanya mazoezi angalau dakika 30 hadi 60 kwa siku au wiki.

Kula mboga mboga na matunda kwa wingi.

Epuka vyakula vilivyokobolewa akwa kula nafaka zisizokobolewa na kutumia aina mbalimbali za mikunde kama maharage, njegere, mbaazi.

Punguza ulaji wa nyama nyekundu yenye mafuta kwa kuoka au kubanika na kul anyama nyeupe kama kuku na samaki.

Epuka mafuta ya wanyama, tumia mafuta ya mimea kama karanga, ufuta na alizeti.

Epuka unyaji pombe uliokithiri na achana na matumizi ya tumabku na bidhaa zake.

Mbwana Samatta aumia tena
Nape ang'ata na kupuliza usalama wa taifa

Comments

comments