Duka kubwa la  Mlimani City (supermarket) Nakumatt lililopo jijini Dar es salaam, limefungwa mapema leo hii baada ya kukosa bidhaa za kutosha kwa muda mrefu na kudaiwa kodi za huduma mbalimbali.

Taarifa ya hiyo imetolewa na Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mroso  na kusema kwamba kabla ya kufungiwa walipewa notisi miezi minne kufanyia marekebisho tatizo hilo.

Meneja amesema kuwa mpaka kufikia siku ya jana hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ndipo walipoamua kuwapa tena notisi nyingine ya mwisho ya siku kumi ambayo ilikuwa inaisha siku ya Jumamosi, na kuamua kuwafungia mapema asubuhi ya leo.

Pastory Mroso ameendelea kwa kusema kwamba tatizo hilo limekuwa likiwaathiri wafanyakazi na hata bidhaa za wafanyabiashara wengine, na pia wamelishalitolea taarifa serikalini ili hatua nyingine ziweze kufuatwa.

 

Serikali kuwatoa sadaka watendaji wazembe
Jose Mourinho asema hatastaafu akiwa Man Utd