Wanawake wengi kwa sasa wanakwenda kuboresha makalio yao ili kuyapatia ukubwa unaostahili kwa jinsi wao wanavyopenda.

Kwa mujibu wa Dk Costantino Mendieta amethibitisha, katika fasihi yake utunzaji wa makalio kwa kuyagawa katika madaraja manne.

Anasema makalio daraja la kwanza ndiyo yanayotakiwa sana Ni kama vile umechukua moyo halafu ukaugeuza chini juu hiyo ndiyo dizaini ya makalio ambayo Marekani wanayapenda sana na wengi hukimbilia katika majumba ya upasuaji kupata shepu hiyo adimu.

Tofauti na kufanya upasuaji unashauriwa kufanya haya kuboresha muonekeano wako.

Fanya masaji na losheni zinazoimarisha na kutengeneza ngozi mwororo katika mapaja yako ukianzia chini ya makalio mara mbili kwa siku.

Ondoa miinuko midogo midogo isiyotakiwa kwa kuskrabu mara mbili au tatu kwa wiki ukitumia salt scrub.

Mazoezi yatakufanya uwe mtu tofauti zaidi pandisha ngazi kwa dakika kumi au zaidi na chukua mazoezi ya kubana makalio yako na sehemu za kiuno kwa kusukuma kwa ndani na kutulia hivyo kwa sekunde tano na kujiachia na unaweza kufanya hivyo unavyotaka.

Pia unaweza kuongeza uzuri wa makalio yako kwa kuhakikisha unakula vyema na unakula inavyostahili.

Abiria waaswa kujinga na Uviko- 19
Safari za ndege zarejea