Maumivu ya korodani  ni tatizo linalowasumbua sana wanaume wengi, kawaida maumivu ya korodani hutokea katika korodani moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi.

Maumivu hayo husababishwa na mambo mbalimbali yakiwemo; maambukizi  ya bacteria au magonjwa ya zinaa, kutokunywa maji mengi, misuguano inayoathiri moja kwa moja ngozi na mirija ya ndani ya korodani ambayo inaweza kusababishwa na uvaaji wa nguo za ndani zinazobana sana, kujikusanya kwa maji na uchafu, ngiri, saratani ya korodani au sababu za kupata ajali.

Hivyo endapo utapata maumivu ya korodani zipo namna kadhaa ambazo mwanaume anaweza kujipatia huduma ya kwanza akiwa nyumbani kama namna ya kutibu maumivu hayo.

Hivyo kama upo nyumbani inashauriwa na madaktari kujitibu kwa kujitahidi kunywa maji mengi na kutotunza mkojo, lakini pia hakikisha unapangusa eneo la korodani zako kwa dakika 5 kwa kutumia maji ya barafu au hata barafu yenyewe.

Pia kwa wale wasio na uwezo wa kupata maji ya barafu chemsha maji yawe vuguvugu kisha weka chumvi kidogo, jikande taratibu kwa dakika 5.

Baada ya kufanya hivi endapo maumivu bado yanasumbua basi fika hospitalini haraka ili ufanyiwe uchunguzwe na kusaidiwa.

Video: Zitto afichua 'Sumu' ya Dk Slaa kwa Lissu, Kina Membe, Nape njiapanda
Hakimu akamatwa kwa wizi wa madawa ya kulevya, alimfunga mtuhumiwa miaka 30