Ngozi kavu huweza kutibiwa na kurejeshwa katika hali yake ya kawaida. Pia mtu anaweza akaitunza ngozi yake na kuikinga isiwe kavu. Hayo huweza kufanikishwa kwa kufanya yafuatayo.

Kupaka mafuta ya kutosha yenye uwezo wa kuongeza maji na kutunza unyevu wa kutosha na kuifanya iwe na maji ya kutosha. Vipodozi unavyoweza kutumia hapa ni Losheni zilizoandikwa MOISTURIZER, mafuta yaliyoandikwa PETROLEUM JELLY, au Glycerine, Kunywa maji ya kutosha kila siku ili yafike na kukaa kwenye ngozi na kuitunza

Kula lishe bora (mlo kamili) na ya kutosha kila siku ambayo itasaidia kuijenga na kuilinda ngozi vizuri (Vyakula vya wanga, protini, mafuta, nyuzi nyuzi, vitamini, madini na maji ya kuosha.

Kupaka vipodozi vinavyoendana na ngozi kavu na vilivyotengenezwa mahususi kwa ajili ya ngozi kavu. Kwa mfano tumia mafuta au losheni zilizoandikwa FOR DRY SKIN.

Epuka jua na joto kali. Unaweza kufanya hivi kwa kufunika vizuri mwili wako, kupaka vipodozi vinavyoukinga mwili dhidi ya miale mikali ya jua (SUN BLOCKERS/SCREENS) , kuepuka kushinda au kufanya kazi juani, kuoga mara kwa mara.

Epuka vipodozi vikali na kemikali zingine vinavyoharibu ngozi na kuikausha. Usiogee sabuni kali, usipake mkorogo, losheni, krimu na mafuta makali kwa ngozi na pia usichubue ngozi.

Mahakama yaamuru Lulu Michael kuachiwa huru
Utaitambuaje ngozi yako kuwa ni kavu? soma hapa