Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ‘TPLB’ imefanya mabadiliko ya ratiba ya michezo ya Namungo FC ambayo inakabiliwa na jukumu la kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema mabadiliko hayo yamefanywa ili kuwapa fursa ya kutosha Namungo FC kujiandaa na mchezo wao wa pili kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri utakaochezwa Machi 17, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Namungo FC ilikua na mchezo wa Ligi Kuu Machi 11 ambayo ni jana, lakini ilikuwa safarini kutoka nchini Morocco walipokua wanakabiliwa na mchezo wa kwanza hatua ya Makundi dhidi ya Raja Casablanca.

Mchezo mwingine ulioahirishwa kwa Namungo FC ulipaswa kuchezwa Machi 17, ambayo inagongana na siku ya mchezo mzunguuko wa pili wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Hivyo Namungo watacheza viporo vya michezo hiyo.

Namungo FC inashiriki kwa mara ya kwanza Michuno ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’, huku ikiwa kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakimiliki alama 27.

Kim Poulsen: Tutaitumia Kenya kutambua udhaifu wetu
Njaa yasababisha watoto kulishwa udongo