Wawakilishi wa Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi Namungo FC, leo usiku watacheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi D dhidi ya Raja Casablanca.

Namungo FC ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo wanakutana na wenyeji wao ambao ni wazoefu katika michuano hiyo waliwahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2018 lakini pia, 2019-2020 walifika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Raja Casablanca imewahi kufika hatua za juu kwa vipindi tofauti na ni moja ya timu kubwa za Morocco zenye mafaniko makubwa kila msimu. Kwa sasa inaongoza ligi kwa pointi 19 katika michezo tisa ikiwa ni timu pekee haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Huenda wenyeji wakawadharau Namungo FC kwa sababu ni timu ngeni, lakini endapo wawakilishi hao wa Tanzania wakijipanga vizuri kwa kuwaheshimu wanaweza kuushangaza ulimwengu wa soka.

endapoNamungo FC watapata ushindi ama sare ugenini, yatakua matokeo mazuri wanarudi kujipanga kwa ajili ya michezo mingine ya Kundi D. 

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI NAMUNGO FC.

Nchimbi aondolewa Taifa Stars
NBS: Mfumuko wa bei umepungua