Mganga wa kienyeji mwenye umaarufu mkubwa nchini Ghana Nana Kwaku Bonsam, ameitabiria mabaya klabu ya Man Utd ambayo kwa sasa inaongozwa na meneja kutoka nchini Ureno Jose Mourinho.

Nana alitangaza utabiri wake kuhusu Man Utd alipohojiwa na kituo cha redio cha Kasapa FM, ambapo alisema Mourinho amekua ni mtu wa majivunio na dharau jambo ambalo linaendelea kumshusha siku hadi siku.

Nana amesema Mourinho ataendelea kuona Man Utd ikipata matokeo mabaya kutokana na dharau alizowahi kumuonyesha aliyekua daktari wa kikosi cha Chelsea Eva Carneiro.

Amesema salama ya meneja huyo na kikosi chake cha mashetani wekundu, ni kuhakikisha anamuomba radhi Eva Carneiro, na kama ataendelea na dharau ya kushindwa kufanya hivyo mabalaa zaidi yatamfika na katu hatoweza kufikia lengo la kuipaisha Man Utd ambayo inahaha kurejesha makali yake.

Image result for Eva CarneiroEva Carneiro

“Jose Mourinho ni mtu wa majivuno, dharau na wakati mwingine hujiona hakuna mwingine kama yeye, huenda ikawa kweli lakini kwa kosa alilolifanya kwa yule daktari wa Chelsea litamtesa sana.

“Licha ya kufanya usajili wa wachezaji wenye hadhi kubwa duniani kama Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic, bado ataendelea kugubikwa na mabalaa makubwa, na hakuna njia ya mkato zaidi ya kuomba radhi na kujutia makosa aliyoyafanya.”

Jose Mourinho wakati akiwa Chelsea aliwahi kumbwatukia aliyekua daktari wa kikosi cha kwanza Eva Carneiro, na taarifa nyingine zinadai alimtusi baada ya kuchukizwa na kitendo cha kwenda kumtibu Eden Hazard bila ridhaa yake, wakati wa mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2015/16 dhidi ya Swansea city ambao ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Bilionea wa Unga 'El Chapo' asimulia mateso anayopata gerezani
Ivan Rakitic Atamani Kuwa Mtumishi Wa Guardiola