Mrembo wa video za muziki na filamu  Tanzania , Nana amefunguka ugumu anaopitia katika sanaa yake ya kuigiza .

Akizungumza mbele ya Kamera ya Dar 24, Nana amesema kuwa anapata shida sana kuigiza kipande cha mapenzi katika kazi yoyote anayopata , kwani anajisikia huru kufanya hivyo na mume wake pekee.

“Napata ugumu kuigiza scene ya kuwa romantic kwasababu sijawahi kufanya hivyo na mwanaume mwingine yeyote tofauti  na mpenzi  wangu , inakuwa ngumu   sio rahisi ‘kukisi’ unajua eeh, au kuigiza kulia sio kitu rahisi,” alisema mrembo huyo .

Nana amesema kuwa mbali na kutopenda kuigiza mambo ya mapenzi, anafurahia sana kufanya kazi kwa ratiba na ushirikiano toka kwa wasanii wenzake .

Angalia mahojiano kwa kina hapa:

Tetesi za usajili: Thomas Partey anukia Arsenal, Inter Milan yamuwania Kante
Ndanda FC yajizatiti kurudi Ligi Kuu 2021/22