Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga maarufu kwa jinà la Nandy amefunguka mwanzo mwisho kuhusu malengo yake ya kuachana na mziki na kuhamishia nguvu zake kwenye biashara.

“Mimi katika ndoto zangu ni kuwa mfanya biashara mkubwa sana na hata wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo baada ya miaka mitano nitacha muziki niendeleze biashara zangu na hadi sasa nimeitumia miaka miwili tu 2016 na 2017” Amesema Nandy.

Nandy amesema kuwa mwaka 2020 aacha muziki na siyo kwamba atakuwa hatoi nyimbo bali atakuwa anatoa kwa mwaka hata mara moja, Pia amesema kuhusu ‘show’ atakuwa anafanya kwa mwaka mara moja ili apate muda wa kusimamia baishara zake.

Nandy ni mwanamziki ambay ameshika kasi katika muziki wa bongo fleva kwa nyimbo kadha ukiwemo wimbo wake wa ‘Ninogeshe’.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 18, 2018
Cape Verde waanika rasmi tarehe ya kuikabili Taifa Stars

Comments

comments