Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Faustina Charles maarufu kama Nandy ameingia ubia na kampuni ya vipodozi nchini ya Grace Products kwa kuzindua bidhaa yake ya sabuni inayoitwa Nandy Beuty soap na mafuta ya kupata ya Nandy Petroleum Jelly.

Nandy amesema ameamua kufanya uzinduzi huo kwani amekuwa akisumbuliwa na watu mbalimbali wakihoji juu ya mafuta anayoyatumia kutokana na mwonekano wake wa ngozi kuwa asilia jambo lililomfanya apate wazo wa kuanzisha bidhaa hizo kwa kina dada.

”Nimekuwa nikisumbuliwa kwa muda mrefu na watu juu ya mafuta ninayotumia, lakini sikuwahi kuwaambia ukweli kwani ningetaja kuwa ni mafuta ya Grace production ningekuwa nimefanya tangazo na mimi ni msanii lakini pia swala hilo limenifanya nipate wazo la kuingia ubia na kampuni hiyo” amesema Nandy.

Hata hivyo wasanii wa muziki wa kisasa wamekuwa wabunifu sana hasa kwa kutumia muziki wao na majina yao kama ‘brand’ za biashara tofauti ambapo swala hilo linawatofautisha na  wasanii wa zamani ambao walikuwa wakitegemea kazi zao za sanaa tu katika kuingiza kipato hali iliyochangia muziki wao kufa mapema.

Mbali na Nandy kuzindua bidhaa zake Ali Kiba naye ni msanii mkubwa sana ambaye ameingia ubia na Rockstar kufanya biashara ya kinywaji cha Energy drink kinachojulikana kama Mo faya, ni hatua nzuri inayochukuliwa na wasanii kwani muziki hauwezi kudumu milele.

Japo Bongo Movie bado hawajaanza kubutuka kutumia sanaa za maigizo yao na filamu zao kutengeneza pesa kwa njia tofauti kitu ambacho kinafanywa sana na nchi zinazofanya vizuri katika tasnia ya filamu kama Marekani ambapo kila bdhaa inayoonekaa katika filamu basi hulipa kiasi fulani cha pesa kwani wameitangaza bidhaa hiyo, wasanii na wafanyabiashara wafunguke katika hilo waanze kutumia fursa.

Video: Watoto 4000 majumbani kuanzishiwa tiba ya saratani
Harusi ya kifalme ya zaidi ya Sh. 100 bilioni kushuhudiwa kesho

Comments

comments