Mkali wa ‘Kivuruge’, Nandy amevurugwa na video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha akiwa mtupu na mwanaume faragha.

Mwimbaji huyo amekiri kuwa video hiyo ni ya kweli na kwamba ilichukuliwa mwaka 2016 kwa makubaliano ya kuwa video ya siri kati yake na mwanaume huyo aliyekuwa mpenzi wake, lakini ameshtuka kuiona leo mitandaoni.

Nandy ameomba radhi kanisa lake, Serikali na mashabiki kwa ujumla kwa kuonekana kwa video hiyo ambayo amesema ilichukuliwa kwa mtindo wa spapchat. Alimrushia lawama mpenzi wake huyo aliyedai ametaka kumchafua.

“Sielewi ana maana gani kuitoa video hiyo kwa sasa na kuifikisha kwenye mitandao kwani vitu hivi vinafanyika kwa mtu yeyote aliye kwenye mahusiano,” aliiambia Mwananchi.

“Naomba radhi kwa mashabiki wangu, kanisani kwangu na serikali. Kwakweli video imenichafua sana ila adhabu ya maumivu haya ninayoyapata sasa hivi ni kutokana na kuamini mtu,” aliongeza.

Aidha, mwimbaji huyo wa THT alidai kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza, kwani aliwahi kuwa na mahusiano na mwanaume ambaye alitaka kusambaza picha zake za utupu lakini alifanikiwa kumzuia baada ya kuripoti polisi.

EXCLUSIVE: Tazama One the Incredible akiichambua mistari ya wimbo wake wa "Adoado Mixer"
Amshambulia mkewe kwa mapanga kisa kunyimwa unyumba

Comments

comments