Msanii wa muziki nchini, Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy rasmi amefunguka kuhusu mahusianao yake na marehemu Boss Ruge ambapo ilitarajiwa mwezi March mwaka huu wangefunga ndoa amabayo ingehudhuriwa na watu wengi wakubwa na maarufu hapa nchini na nje ya nchi pia.

Nandy amekiri kuwa na mahusiano mazito na Boss Ruge yaliyodumu kwa takribani miaka mitatu, na tayari wawili hao walikuwa wametambulishana na kukubalika kwa wazazi wa pande zote mbili.

Ametaja sababu ya kutoweka mahusiano yao mitandaoni na kusema kuwa hawakupenda mahusiano yao yaendeshwe na mitandao kwani walijua madhara makubwa yatokanayo na tabia ya kuweka mahusiano kwenye mitandao ambayo kwa kiasi kikubwa yangepelekea wawili hao kutotimiza mipango yao kimaisha.

”Tumeoana madhara, Yeye alishawahi kuweka mahuasiano yake wazi,… yalikuwa na maneno, drama, kipindi ambapo sipo nae nilikuwa naona, so hatukutaka hiyo life style iendelee tena kwenye maisha yetu” Amesema Nandy.

Aidha kabla ya kifo cha Boss Ruge, Nandy amekuwa akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kukana kuwa kimahusiano na Boss Ruge na kudai kuwa Ruge ni Boss wake na mtu anayemsaidia kusimamia kazi zake za muziki.

Rugemalira Mutahaba kipindi cha uhai wake alikuwa ni mkurugenzi wa uzalishaji vipindi Clouds Media ambaye alifariki dunia mwishoni mwa mwezi wa Pili akiwa Afrika Kusini kwa matibabu ya maradhi ya figo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine UDOM
INBAR Yaitaka Tanzania kuweka mkazo kwenye biashara ya Mianzi

Comments

comments