Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Faustina Charles ‘Nandy’ amepokea Cheti kutoka Studio za Academy Recording ya waandaaji wa Tuzo za Grammy, ya kutambua mchango wa ushiriki wake katika album ya mwanamuziki mahiri kutoka nchini Jamaica Etana “Pamoja”.

Albam hiyo, ambayo imemfanya Nandy kuingia kwenye machapisho ya habari kubwa za vyombo mbalimbali vya Habari za Dunia kutokana na uwezo wake kimuziki, ambapo iliingia kwenye kinyang’anyiro cha album bora ya Reggae, mapema mwaka 2021.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Nandy ametoa shukurani zake za dhati kwa Studio za Academy Records kwa kuthamini mchango wake kupitia wimbo huo alioshirikishwa na mwimbaji Etana.

“Ahsante Recording Academy kwa Kushirikishwa kwenye wimbo na Etana strongone (PAMOJA) iliyokuwa ulioteuliwa na GRAMMY katika Album bora ya Reggae,” ameandika Nandy.

Kenya: Mahakama yafungwa ili kusikiliza kesi ya uchaguzi
Watawa wa RC waliotekwa nyara waachiliwa huru