Mkali wa ‘One Day’ aliyetisha kwenye jukwaa la Tecno Own The Stage nchini Nigeria, Nandy amewaweka kando ya maelezo marapa wawili, Dogo Janja na Bill Nas waliokuwa wakivuma kwenye tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo huyo.

Nandy ambaye aliwahi kuweka wazi kuwa anatafuta mpenzi, alipiga stori na Lil Ommy wa The Playlist ya 100.5 Times FM na kukana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na yeyote kati ya marapa hao.

Hata hivyo, nafasi bado iko wazi kwa mrembo huyo aliyedai kuwa tangu alipoweka wazi kuwa anatafuta mpenzi bado hajapata wa kuichukua nafasi hiyo.

Mrembo huyo aliweka wazi vigezo kadhaa vya mwanaume atakayeziba nafasi ya moyo wake wa kumuita ‘mahabuba’.

“Kikubwa awe mcha Mungu, muelewa, mvumilivu… kutesana hivyo ni vitu vya kawaida lakini akiwa mvumilivu ina maana hata mimi nitakuwa mvumilivu kwake,” Nandy alifunguka.

Katika hatua nyingine, Nandy alisema kuwa ujumbe wake kwenye wimbo wa ‘One Day’ haukuwa simulizi la kweli la maisha yake bali alitaka kufikisha ujumbe unaoakisi hali ya mapenzi katika jamii.

Nandy alimuweka baba yake mzazi kwenye video ya ‘One Day’ iliyoongozwa na Destro

TFF Yampeleka Hajji Manara Kamati Ya Maadili
FC Barcelona Kumpigania Neymar CAS