Wasanii wa muziki wa bongo fleva akiwemo Diamond Platnumz, Rayvanny na Nandy wamefanikiwa kushinda tuzo za #aeausa2020 kwenye vipengele tofauti tofauti zilizotolewa nchini Marekani.

Mbali na Diamond Rayvanny na Nandy kushinda tuzo pia DJ Sinyorita kutoka Clouds Fm amefanikiwa kushinda tuzo ya DJ bora wa mwaka.

Diamond ametangazwa mshindi tuzo za @aeausa 2020 katika kipengele cha “Best Male Artist” (Msanii Bora wa Kiume) akiwashinda Eddy Kenzo, Wiz Kid , Shatta Wale, Stonebwoy, Davido, Burna Boy, Mohamed Abbas, Fally Ipupa na Jahllano ambao alikuwa akichuana nao kwenye Kipengele hicho.

Huku Rayvanny akitangazwa mshindi tuzo za @aeausa 2020 katika kipengele cha Best Male Artist – East/South and North Africa akiwashinda Elgrande toto, The Ben, Diamond Platnumz, Alikiba, Eddy Kenzo, Harmonize, Tewodros kassahun AKA Teddy Afro, Jah Prayzah na Bruce Melodie.

Kwa upande wa Nandy ametangazwa mshindi tuzo za @aeausa 2020 katika kipengele cha “Best Female Artist” akiwashinda Zahara, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sho Madjozi, Sha Sha, Sheebah Karungi, Rema Namakula, Aya Nakamura na Kenza Morsli .

DJ pekee kutoka Tanzania DJ Sinyorita ameshinda kipengelea cha DJ bora akiwashinda DJ Moh, DJ Cuppy.

Mawakili wapotoshaji waonywa
FC Platnum yaitega Simba SC