Moja kati ya gari la msafara wa msanii Nandy limepata ajari wakiwa njiani kuelekea mkoani Sumbawanga kwaajili ya kutumbuiza siku ya Eid mosi mkoani hapo.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa msanii Nandy ni kwamba baadi ya watu walioumia katika ajali hiyo wamerudi  jijini Dar es salaam kwaajili ya matibabu huku wengine wakiendelea na msafara kuelekea Sumbawanga.

Nandy ametuma video fupi katika ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa miongoni mwa watu walioumia ni wanenguaji, viongozi na baadhi ya watu wengine waliokuwa kwenye gari hiyo huku majeruhi wakirudishwa jijini Dar es salaam kwaajili ya matibabu.

Amewaomba mashabiki wa Sumbawanga wasiwe na wasiwasi, wasanii wanakuja kwaajili ya show ya Eid mosi huku mmoja kati ya wasanii ni kutoka nchini Kenya anaejulikana kama Willy Poul ambaye ameshirikishwa na Nandy katika wimbo wa Halleluya.

Idadi ya wagonjwa wa Dengue yapaa, 3 wafariki dunia Dar
Bei ya mahindi Kenya yapaa, Viwanda 10 vyafungwa

Comments

comments