Shirika la afya la duniani (WHO) limesema ni watu wachache pekee wanafaa kuvaa barakoa, ambao ni wanaoumwa na wanaoonyesha dalili, na mhudumu wa watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Corona.

Na katika hospitali barakoa za aina tofauti zinatoa ulinzi wa viwango tofauti, inayotoa ulinzi bora zaidi ni FFP3 au N95 au FFP2 ina kifaa cha kupumilia ambacho uchuja hewa mtu anayovuta.

Barakoa za upasuaji hazijapendekezwa kwa matumizi ya umma kwasababu zinaweza kuchafuliwa na kikohozi vya watu wengine au unapopiga chafya au unapoivaa na kuivua.

Wataalam hawashauri umma kutumiwa hizi ni kwa ajili ya wahudumu wa afya ambao wapo karibu zaidi na wagonjwa wa corona na wapo katika hatari kubwa ya kukumbana na majimaji ya njia ya hewa kutoka kwa waathirika.

Virusi vya Corona vinaweza kusambazwa kwa matone ambayo yanaweza kusambaa hewani, pale ambapo wale walioambukizwa wakiongea, wakikohoa au kupiga chafya, lakini kama hawa watu wakivaa barakoa haya matone yanaweza kupunguzwa.

Virusi hivyo vinaweza kuingia mwilini kupitia macho na mdomo au baada ya kugusa vitu vilivyopata maambukizi.

Taarifa hiyo ya WHO, imeeleza kuwa haishauriwi kutumia barakoa iliyotengenezwa nyumbani kwa sababu hakuna uhakika kuwa itatoa kinga ya kutosha au la.

Hata kama barakoa hizo za nyumbani zikitumika kwa usahihi, lakini kitambaa hakijathibitishwa kuwa na ubora wa kinga hivyo ni vinaweza kuwa hatari kwa maambukizi.

Mambo yafuatayo yanashauriwa kufuatwa ili kujilinda dhidi ya virusi vya Corona;

  • Nawa mikono kwa maji na sabuni mara Kwa mara, angalau kwa sekunde 20 na mara tu baada ya kurudi nyumbani
  • Tumia sanitizer kama hakuna maji na sabuni
  • Ziba mdomo wako kwa tishu au kitambaa na sio mikono yako ukiwa unapiga chafya ,weka tissu uliotumia katika pipa la taka na unawe mikono yako
  • Usishike Macho,pia au mdomo kama mikono yako michafu
UEFA yatahadharisha wanaomaliza ligi mapema
Fàbregas awakubali Wenger, Mourinho

Comments

comments