Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amempa mkono wa kwaheri aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Abdulrahman Kinana aliyejiuzulu nafasi hiyo jana.

Nape ambaye amefanya kazi kwa karibu na Kinana kwenye harakati za chama akiwa kama Katibu wa Itikadi na Uenezi, amekumbuka mabadiliko makubwa aliyoyaleta kwenye chama hicho.

Akiambatanisha picha inayomuonesha akiwa na Kinana pamoja na January Makamba kwenye akaunti yake ya Twitter, Nape ameikumbuka mbegu ya mtazamo chanya na tofauti juu ya siasa aliyoipanda ndani ya chama hicho na kuahidi kuwa itaota.

“Pumzika Rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! TUTAKUENZI DAIMA! Cde. Kinana! Umepanda mbegu na ITAOTA!” ameandika.

Uamuzi wa Kinana ulitangazwa jana na kuridhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli aliyemshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kujenga chama.

Akizungumzia sababu za kujiuzulu, Kinana alisema kuwa amefikia hatua hiyo kwakuwa anahitaji kupumzika baada ya kufanya kazi ya chama kwa muda mrefu.

 

Lukuvi afikisha ujumbe mzito kwa wamiliki wa ardhi
Wema Sepetu kufanyiwa upasuaji India