Aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa siasa sio uadui hivyo wananchi na baadhi ya viongozi wanapaswa kuelewa hilo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha habari cha CloudsTv, ambapo amesema kuwa wanasiasa wengi wa upinzani ni marafiki zake hivyo kuwa mpinzani sio kuwa adui.

Amesema kuwa raha ya siasa ni kushindana kwa hoja na wala si kujenga uadui kwani kuna maisha baada ya siasa ambazo zimekuwa zikigusa hisia za watu mbalimbali na kuamini kile ambacho sera yao inawaongoza.

”Mfano mzuri ni mimi hapa, nina marafiki wengi sana wa upinzani, huwa tunashindana sana kwa hoja kulingana na sera ya chama, lakini baada ya kumalizika tu kwa uchaguzi, mimi na rafiki zangu akina Lowassa, Zitto huwa tunakuwa pamoja,”amesema Nape

Hata hivyo, ameongeza kuwa hawezi kuklinganishwa na kiongozi yeyote wakati wa kipindi chake cha uongozi wake kwakuwa kila dhana ina wakati wake wa utawala katika eneo husika na kwa kipindi maalumu.

Chid Benz amshauri Makonda, 'huwa tunatakaga hela'
Video: Mdee: Damu ya Lissu haitawaacha salama, Fatma Karume sasa atoa msimamo