Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini kuwa haifanyi kazi zake ipasavyo na inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania

Ameyasema hayo bungeni wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma.

Nape ameishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali na kukumbuka jukumu lao la kuhakikisha wanalinda uchumi wa nchi katika kipindi hiki ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi.

Hata hivyo, kwa upande Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika amesema kuwa kazi ya usalama wa Taifa wa nchi yeyote ni kutafuta habari na kuishauri serikali. Kwa kifupi.

Najitambuaje nina Saratani? soma yafuatayo
Miguna adai atamng'oa Kenyatta madarakani

Comments

comments