Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa, na Michezo, Nape Nnauye amewataka wananchi kuunga mkono  juhudi za Serikali katika uwekezaji hapa nchini na kuwaeleza wanaobeza  uwekezaji hwajui walitendalo, amesema hata nchi zilizo endelea kama Marekani zinahamasisha uwekezaji.

Ameyasema hayo alipokuwa alipokuwa akizindua ushirikiano wa pamoja kati ya wanahabari wa China na Tanzania na kufanya mahojiano na wawekezaji kutoka China, ambapo amesema wanaobeza  uwekezaji ipo siku watatambua umuhimu wa uwekezaji huo hapa nchini.

Nape amesema China ni nchi yenye uwekezaji mkubwa kuliko nchi yoyote katika Bara la Afrika, hivyo ushirikiano wa wanahabari  utsaidia kueleza ukweli kuhusu uwekezaji wa Afrika kupambana na propaganda za nchi za Magharibi kuwa bara la Afrika lina mambo mabaya pekee.

Rungwe amgeukia Profesa Lipumba
Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020