Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kushirikiana na Serikali kwa kupeleka michezo mbalimbali ikiwemo soka kwenye mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kufanyika mjini Tokyo Japan mwaka 2020 ili kupata nafasi ya kushinda.

Hayo yamesemwa mapema hii Jijini Dar es Salaam  alipokutana na wadau wa soka katika muendelezo wa kipindi chake  cha “Wadau  Tuzungumze” lengo ikiwa ni kujadili namna ambavyo timu ya mpira wa miguu itakavyoweza kushiriki katika mashindano hayo ya Kimataifa.

Amesema kuwa, ushiriki wa timu za mpira wa miguu kwenye mashindano ya  Olimpiki ni muhimu katika kukuza na kuendeleza soka huku akiwataka wadau hao kupeleka michezo mingi zaidi ili kupata nafasi ya kushinda medali mbalimbali.

“ Lengo  letu ni  kupata ushindi hivyo kwa kupeleka michezo mingi katika mashindano haya ya Olimpiki tunajitengenezea nafasi nzuri ya kurudi na ushindi  na kuondokana na dhana ya kuwa washiriki,” amesema Nape

Aidha amewataka watanzania kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha  ushindi unapatikana ikiwemo  kuwapa moyo wachezaji wetu kupitia uhamasishaji wa wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

kamati hiyo inaoongozwa na Charles Hillary   wajumbe wengine ni pamoja na Selestine Mwesigwa, Beatrice Singano,Hassan Abbas, Ruge Mutahaba, Hoyce Temu, Eric Shigongo, Maulid Kitenge, Naseeb Abdul (Diamond) na Ally Kiba.

Kwa upande wake Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alfred Lukas ameahidi na kueleza kuwa safari hii watahakikisha timu zitakazokwenda kuwakilisha katika mashindano ya Olompiki Mjini Tokyo Japan hawaendi tu kushiriki bali kurudi na ushindi na kuitangaza Tanzania kupitia michezo.

 

Serikali kuwajengea uwezo wanawake kutumia teknolojia
Yusuph Mlela aikosoa tasnia ya filamu