Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezua gumzo ndani na nje ya Bunge wakati akitoa mchango wake ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu.

Nape alieleza kutoridhishwa na kukosekana kwa suala ya gesi ya Mtwara na Lindi kwenye hotuba hiyo ingawa imeonekana kwa undani kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015.

Alisema kuwa Ilani hiyo ndiyo mkataba kati ya CCM na wananchi walioipa kura za kuingia madarakani na gesi ya Mtwara inaonekana katika ukurasa wa 74 na 75.

Mbunge huyo alidai kuwa baada ya kuachwa kwa suala hilo, maisha ya wananchi wa Mtwara na Lindi yamekuwa magumu na wawekezaji ambao walikuwa wamepiga kambi wakijua kuna fursa ya gesi kama ilivyoahidiwa wameanza kundoka.

“Ni bahati mbaya kwamba hili suala humu ndani hakuna kabisa, maana yake ni kwamba hili jambo pengine limeanza kuachwa sasa twende Stiegler’s, lakini hatuisaliti Ilani ya uchaguzi ya CCM?” Alihoji.

Nape aliongeza kuwa waliamini kuwa kwa bahati nzuri Waziri Mkuu aliyechaguliwa anatoka Lindi, hivyo wangekuwa salama kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, Nape alipata wapinzani wa kauli yake ndani ya Bunge hilo, ambapo Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alikosoa kauli ya Nape kuhusisha maendeleo na anakotoka Waziri Mkuu.

Lusinde alisema kuwa kauli hiyo inaashiria kuwaangalia viongozi na maendeleo kwa kanda wanazotoka, jambo ambalo sio sahihi. Alisema Waziri Mkuu ni wa Tanzania nzima kama ilivyo kwa Rais hivyo kuangalia kanda anayotoka sio sahihi. Kauli ya Lusinde iliungwa mkono na Mbunge wa Geita vijijini, Joseph Msukuma.

Mchango wa Mbowe na walioupinga ulitua tena kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo na midahalo isiyo rasmi.

IGP Sirro, Wangabo watimiza ahadi yao kwa wakazi wa bonde la ziwa Rukwa
Msafara wa Mayweather washambuliwa kwa risasi.