Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa anapoyakumbuka maisha ya changamoto za miundombinu kwa wananchi wa mikoani aliyoyashuhudia huonekana mkorofi.

Nape ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kueleza hisia zake akiweka picha inayoonesha wananchi wakivuka mfereji mkubwa wa maji machafu kwa kupita ndani ya maji hayo.

“Niliyashuhudia maisha haya mikoani(38 months), nadhani ndio nikiyakumbuka naonekana mkorofi!!Iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu!” aliandika Nape.


Katika tweet nyingine, Nape aliweka picha ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwa amepanda mtumbwi na nyingine akiwa anashiriki kuvuna mtama na baadhi ya wananchi, na kueleza kuwa hayo ndiyo yalikuwa maisha ya miezi 38 (miaka mitatu) bila kufafanua zaidi.

“Haya ndio yalikuwa maisha kwa miezi karibu 38! Big up Cde Kinana,” aliandika.


Nape alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri na kuachia nafasi hiyo iliyochukuliwa na Humphrey Polepole.

Korea Kaskazini Yatoa Vitisho Vingine Vizito Dhidi Ya Marekani
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma muda huu